Followers

Friday, January 2, 2009

Vimbwanga Time hewani leo Channel Ten

Kikundi kipya cha magizo ya vichekesho cha Vimbwanga Time leo kitaanza rasmi kurusha vichekesho vyake kupita kituo cha Televisheni cha Channel Ten cha jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa kikundi hicho Dennis Rupia amesema kipindi chao kitajulikana kwa jina la Vimbwanga Time na kitakuwa kikirushwa kila Jumamosi saa 2:00 hadi saa 3:00 usiku na kurudiwa Jumapili saa 10: 00 hadi 11:00 jioni katika kituo hicho hicho.
“Vimbwanga ni kikundi kipya ambacho kinaundwa na wasanii chipukizi katika fani ya vichekesho hapa Tanzania, tunafanya komedi zenye mwelekeo unaoendana na maisha ya kawaida na ya kila siku katika jamii,” alisema Denis.
Amesema kikundi hicho kinaundwa na wasanii saba, lakini pia kinatumia wasanii wengine ambao huwa kinawaalika kulingana na mahitaji. Amewataja wasanii hao na majina ya kisanii kwenye mabano kuwa ni pamoja na Grace Simba (Fet), Yona Chibaruwa (Profesa Kudeche), Jumanne Mgalike (Tumbo), Miraji Mnako (Dkt. Panjuan), Salum Digale (Yatman), Kudura Luselo (Kidy) na yeye Denis (Dedalunde).
Denis amesema kuwa kundi hilo liko chini ya kampuni ya ESMEN Media Pro. Limited ya jijini Dar es Salaam ambapo mtayarishaji wake ni Edwin Ndeketela na muongozaji wa programu ni Hassan Bumbuli.
“Tumejipanga vizuri kutoa burudani na elimu kwa jamii ya Watanzania, tunao watalaamu katika idara muhimu, hivyo watanzania watarajie kuona mambo mazuri na waandae vyema mbavu zao,” amesema.
Amesema kundi hilo limeingia mkataba wa mwaka mmoja na kituo cha Channel Ten kurusha kipindi hicho ambacho kitakuwa cha saa moja.
Lukwangule

1 comment:

  1. Hi Msimbe,

    First I would like to Thank You for accepting my request to become a contributor to this blog and best wishes for Happy New Year 2009 though belated. I hope my other requests will be accepted soon. Thanks for the first contribution. It would grateful if you could post blogs in English so that it can have wide reader-coverage. Even I can't understand what you've written :). However, once again I would like to thank you for your generous contribution.

    With Best Regards

    Flora

    ReplyDelete

My Headlines